Taarifa inasemekana alimjeruhi mwenzake vibaya, ambaye alitibiwa na kupona na alibaki nchini Kenya akiendelea na kazi zingine. Wakati huyo msaliti akiendelea kujichimbia nchini Somalia.
Inaandaliwa operesheni, aliyotakiwa mpelelezi mmojawapo atumwe kwenda huko. Huyo aihitajika kufika mjini Lamu aonane na jasusi aliyejeruhiwa, ambaye angekuja kumsafirisha kwa kutumia watu wake kwenda Juba. Huko wangekuja wapelelezi wengine ambao wangeigiza kama wanamgambo, hao wangemteka na kumfikisha kwenye kundi mojawapo la wanamgambo huko ndiyo angefanya kazi yake.
Shirika lilimteua Norbert Kaila kushikilia jukumu hilo, ambaye aliondoka nchini Tanzania kwa mujibu wa itifaki ilivyo. Ila mambo yanakuja kugeuka baada ya kufika nchini Somalia. Huko anatekwa kibaya zaidi wanaofanya kazi hiyo ni majambazi kamili wa kundi mojawapo, na si wale wenzake ambao walipangwa kufika huko.
Watekaji waliwahi mapema kabla ya majasusi wengine, walitimiza jukumu hilo, mwisho wake ikaja kuwa tatizo kubwa kwa EASA. Norbert Kaila aliwekwa nguvuni, inampasa kujiokoa na kuendelea na misheni yake.
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.








