Hapo ndiyo tamaa ilipomwingia kwa kuliona shamba kubwa, ambalo halikuendelezwa na kujengwa nyumba za kisasa, licha ya mji kutanuka. Kukabaki kuwa vilevile, katikati yake kukiwa na mti mkubwa sana.. eneo ambalo lilimfaa hasa kujengea uwanja wa kisasa wa timu, sababu lipo mahali pazuri.
Alijaribu njia ya kawaida ya kutaka auziwe, ila wamiliki waligoma na kumwambia halitakiwi kuuzwa. Ulikuwa urithi toka enzi, ikitakiwa kubakishwa hivyo kwa vizazi hadi vizazi. Pia wakitakiwa kuumwagia mji mti mkubwa kila atakayesimamia.
Utamwambia nini mwenye mambo ya kisasa kuhusu mila? Ndiyo hapo bilionea akatafuta watu ambao waliamua kutumia mbinu chafu kulipata eneo hilo. Wakaishia kuukata mti ule na kujenga uwanja wa kisasa. Ila baadaye walikuja kujuta na kutamani muda urudi nyuma
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.








