Binti alipokuja kupatikana jasusi naye hakuonekana na wala kutambulika alipo. EASA hawakutaka kulifumbia macho suala hilo. Ilikuwa lazima mtu wao apatikane na sababu ya kutoweka kwake ijulikane. Maana hakuna kuku anayeweza kusahau kwao, kama hajarudi bandani basi amekutwa na jambo linalohitaji msaada wa ziada.
Ndipo hapo alipoteuliwa Norbert Kaila aliyekuwa mapumzikoni nchini humo. Baada ya kumaliza misheni yake aliyokuwa akiifanya Tanzania, akaishia kupewa likizo. Ila napo alikuja kusitishiwa na kutakiwa kurudi kazini, amtafute mwenzake alipo.
Mapya yanakuja kuibuka kwenye kazi hiyo, anapokutana na mtu ambaye alimdhani ndiye kumbe siye
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.